
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Paul Christian Makonda amesisitiza umuhimu wa Vijana na Watanzania kwa ujumla kumlinda Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awakikaribisha wote wanaomtusi na Kumdhihaki Dkt. Samia kumuacha aendelee kuwaletea maendeleo Watanzania, akisema yupo tayari kupambana nao kwaniaba ya Dkt. Samia kwa hoja na Vioja, lengo ni Chama Cha Mapinduzi kiibuke na ushindi.
Makonda amekaririwa akisema;
“Ninaomba niwaulize swali ndugu zangu, wakati Kaka yangu Hayati Magufuli akiwa Rais alifanya kazi ya heshima sana, kiliibuka kikundi kilimtukana asubuhi mpaka usiku na wakati yupo kitandani anapigania uhai wake, kikundi hiki kilimtukana na kumdhalilisha kwa kila aina ya matusi.
…. Leo hii ametangulia mbele za haki, Mungu katupa Dkt. Samia, kikundi kilekile kimeungana kumtukana Dkt. Samia usiku na mchana, Watanzania mpo wapi kumlinda Rais wetu, Vijana mpo wapi wa hamasa kumlinda Dkt. Samia? Mwanza mpo wapi kumlinda Dkt. Samia?
“Wananchi hawa wanakifahamu hicho kikundi na wengi hawakai hapa nchini na nimeona jana wameanza kwenye mitandao kuniandika, mimi ni saizi yenu, mwacheni Dkt. Samia aongoze nchi, njooni tuhangaike na Makonda na mimi nipo tayari kupambana na ninyi kwa kila hoja na vihoja kuhakikisha CCM inashinda.” Amesisitiza Makonda.

