Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
Kardinali Pengo amefariki dunia jana alipokuwa akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Katika salamu zake za pole, Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho, akibainisha kuwa katika kipindi chote cha utumishi wake ndani ya Kanisa Katoliki, Kardinali Pengo alisimama imara kuhubiri amani, maadili na mshikamano wa kitaifa.
Ameeleza kuwa mchango wake mkubwa kwa taifa na kwa waumini wa Kanisa Katoliki utaendelea kukumbukwa na kuenziwa siku zote.
