Nature

Rais Samia Ateua Wabunge Wapya Watano, Majina Haya Hapa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewateua wabunge wapya watano kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses M. Kusiluka, imesema uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo Rais chini ya Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Walioteuliwa ni Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Balozi Khamis Mussa Omar na Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho.

Kwa mujibu wa Katiba, Rais ana mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi kumi ambao, kwa maoni yake, wanaweza kutoa mchango maalum katika shughuli za Bunge.

Uteuzi huu unaongeza nguvu katika chombo hicho cha kutunga sheria, huku wachambuzi wa masuala ya kisiasa wakitarajia kuona wabunge hao wapya wakitoa mchango katika mijadala ya kitaifa na utekelezaji wa sera za maendeleo.

Aidha, uteuzi huo umeonekana kama ishara ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Bunge katika kusukuma ajenda za maendeleo, hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa linaendelea na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

Baadhi ya wananchi na wadau wa kisiasa wameipongeza hatua hiyo, wakisema kuwa majina yaliyoteuliwa yanaonesha dhamira ya Rais Samia ya kuendeleza uwakilishi wa watu wenye uzoefu na taaluma mbalimbali ndani ya Bunge, jambo linalotarajiwa kuongeza ufanisi katika mijadala na usimamizi wa sera za umma.

Related Posts