Nature

Rais Samia Kuchukua Fomu ya Kugombea Urais Leo Dodoma

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgombea mwenza wake Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajia kuchukua fomu ya Urais leo August 09,2025 asubuhi katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi Jijini Dodoma.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema hayo Jijini Dodoma leo August 08,2025 wakati akiongea na Waandishi wa Habari.

“Nimewaita kwa jambo moja kubwa sana, jana Tume ya Uchaguzi imetoa ratiba ya uchaguzi na uchukuaji fomu kwa nafasi mbalimbali, Wagombea Urais kuanzia tarehe 09 hadi tarehe 27 na Madiwani na Wabunge kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 27 na uchaguzi mkuu October 28, tarehe 27 siku ya mwisho ya uteuzi saa 10 jioni”

“Baada ya kupata ratiba hiyo tumepata picha ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, kwa CCM mchakato wa kupata Mgombea Urais Tanzania na Zanzibar ulishakamilika January mwaka huu, nimewaita rasmi kuwajulisha kwamba Mgombea Urais wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi wanaenda kuchukua fomu kesho”

“Kwahiyo Dkt. Samia ndio Mgombea wa Chama chetu, atachukua fomu kwenye Tume ya Uchaguzi hapa Dodoma saa nne na dk 50 na tunatarajia baada ya kuchukua fomu na kupewa maelekezo atakuja ofisi za CCM hapa Makao Makuu na kusaini kitabu na kusalimiana na Wananchi na Wana CCM hapahapa makao makuu ya CCM”

Related Posts