
Huenda Rais wa Marekani Donald Trump akawa ‘Content Creator’ mzuri bila kujijua kutokana na matukio au mazungumzo yake mengi kugeuka gumzo baada ya kuyawasilisha.
Picha ya Rais Trump
Hapa tunakuletea baadhi ya matukio yake manne aliyoyofanya siku za hivi karibuni na kugeuka ‘Content’ nzuri kwa hadhira kuanzia vyombo vya habari mpaka mitandaoni.
– Kumsifia rapa Nicki Minaj Ikulu kusema yeye ndio Malkia wa Rap, mrembo anavutia na ana kucha ndefu ambazo ni nzuri.
Pia akaenda mbali sana kusema anamuona Nicki atakua Mwanasiasa mzuri huko baadae kama akiamua kufanya siasa.
– Kingine kutoka kwake amedhihirisha anauweza Utabiri, baada ya kumtabiria Bondia Jake Paul kwamba atakuwa Mwanasiasa mkubwa huku akiahidi kumpigia debe.
– Trump huyu huyu juzi tu kasema hamjui Messi baada ya kuulizwa na mtoto wake, pia alimtaja Ronaldo mbele ya Messi kama vile umzungumzie Diamond mbele ya Alikiba.
Messi na timu yake MLS ilialikwa Ikulu, wakati wa Speech ya Trump alisema “Mwanangu aliniuliza Baba unajua nani atakuwa huko leo? Nikasema hapana, nina mambo mengi yanayoendelea”.
– Cha mwisho kwa leo wakati ambao dunia inamlaumu kutokana na yanayoendelea Mashariki ya kati, yeye aliamua kuwaalika Wachungaji na viongozi wa dini kutoka Majimbo tofauti nchini Marekani ili wamuombee.
Unadhani Trump anashida gani mpaka atake kuombewa?
