
Rais wa mpito aapishwa Venezueala, Maduro akikana mashitaka Marekani
Delcy Rodríguez amesema aliumizwa na kile alichokiita “kutekwa nyara” kwa Maduro na mkewe
Delcy Rodríguez ameapishwa kuwa rais wa mpito wa Venezuela katika kikao cha bunge kilichoanza kwa wito wa kuachiliwa kwa rais aliyeondolewa na kuzuiliwa nchini Marekani Nicolás Maduro
Rodríguez, 56, makamu wa rais tangu 2018, alisema aliumizwa na kile alichokiita “kutekwa nyara” kwa Maduro na mkewe Cilia Flores ambao walikamatwa na vikosi vya Amerika katika uvamizi wa usiku wa Jumamosi.
Katika matukio ya kushangaza ndani ya chumba cha mahakama jijini New York saa kadhaa hapo awali, Maduro alisisitiza kuwa bado ni rais wa Venezuela huku akikana mashtaka manne ya ulanguzi wa dawa za kulevya na ugaidi.
Marekani imekosolewa vikali mkali Umojnaa wa Mataifa, lakini balozi wa Marekani alisema hifadhi kubwa zaidi ya nishati duniani haiwezi kuachwa mikononi mwa kiongozi haramu, ” mkwepaji haki”.
Kabla ya Maduro kufikishwa mahakamani, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya kikao cha dharura kujadili hali ya Venezuela.
Balozi wa Venezuela, Samuel Moncada, alisema nchi yake imekuwa ikilengwa na “shambulio haramu la silaha lisilo na uhalali wowote wa kisheria”.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz, alihalalisha shambulio hilo kwa kumtaja Maduro kama “rais haramu”
