Nature
Barack Obama Vs Trump

Rais wa Sasa wa Marekani, Donald Trump Atupiana Maneno na Barack Obama

Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump, amemshutumu rais wa zamani wa nchi hiyo Barack Obama kwa kile alichokiita “uhaini,” akidai kuwa alihusika kupanga njama za kuhujumu utawala wake kupitia tuhuma za kuhusishwa na Urusi katika uchaguzi wa mwaka 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, Trump alisema: “Walijaribu kuiba uchaguzi. Obama alitaka ushindi wangu usitambuliwe.”

Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya ripoti kutoka kwa Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa wa Marekani, Tulsi Gabbard, kudai kuwa kulikuwa na njama za ndani ya serikali ya Obama kupanga kile kinachoitwa “mapinduzi dhidi ya Trump.”

Ripoti hiyo imetupiliwa mbali na chama cha Democrats wakisema haina msingi wa kweli. Msemaji wa rais wa zamani Barack Obama alijibu shutuma hizo kwa ufupi, akizitaja kama “jaribio dhaifu la kuvuruga umma.”

Tuhuma hizo zimezua mjadala mpya wa kisiasa, hasa wakati huu ambapo Trump anatafuta muhula mwingine wa urais kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa baadaye mwaka huu.

Wakati huohuo, Trump anakabiliwa na maswali yanayozidi kuongezeka kuhusu kifo cha Jeffrey Epstein — mnyanyasaji wa kingono aliyefariki gerezani mwaka 2019 akiwa anakabiliwa na mashtaka ya kuendesha mtandao wa usafirishaji wa wasichana kwa ajili ya ngono.

Mashinikizo kutoka kwa umma na vyombo vya habari yanaongezeka kutaka utawala wa Trump kufichua nyaraka na taarifa zaidi kuhusu kifo cha Epstein na uhusiano wa viongozi wakubwa wa kisiasa katika sakata hilo

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *