Rais wa Shirikisho la Soka la Congo DR Ahukumiwa Kifungo cha Maisha Jela

Rais wa Shirikisho la Soka la Congo DR Ahukumiwa Kifungo cha Maisha Jela
Rais wa Shirikisho la Soka la Congo DR Ahukumiwa Kifungo cha Maisha Jela

Rais wa Shirikisho la Soka la Congo DR (FECOFOOT), Jean-Guy Blaise Mayolas, amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa uchakatishaji pesa , utengenezaji wa nyaraka za uwongo, pamoja na ubadhilifu wa pesa za FIFA zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya soka la wanawake na ujenzi wa vituo vya michezo.

Uchunguzi ulibaini kuwa Mayolas alitumia karibu dola milioni 1.3 za fedha za FIFA kwa manufaa yake binafsi, na kutumia mtandao wa miamala ya kifedha ya bandia na rekodi za uwongo kuficha ukweli huo.

Mke na mwanawe pia wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuhusika na makosa hayo. Katibu Mkuu wa FECOFOOT, Badji Mombo Wantete, na Mhasibu, Raoul Kanda, wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kila mmoja

Related Posts