Nature

Rais wa zamani wa DRC, kabila ahukumiwa adhabu ya kifo na mahakama ya kijeshi kwa kosa la usaliti

Mahakama ya kijeshi DRC imemhukumu kifo aliyekuwa rais Joseph Kabila, ikimtia hatiani kwa usaliti na uhalifu dhidi ya binadamu. Chama chake PPRD kimesema kesi hiyo ni ya kisiasa dhidi ya mpinzani mkubwa wa serikali

Mahakama ya kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imemhukumu kifo aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila, bila mwenye kuwepo, baada ya kumtia hatiani kwa makosa kadhaa mazito yakiwemo usaliti na uhalifu dhidi ya binadamu.

Hukumu hiyo imetolewa Jumanne na Luteni Jenerali Joseph Mutombo Katalayi, aliyesimamia shauri hilo katika mji mkuu Kinshasa. Jaji huyo alisema Kabila, mwenye umri wa miaka 54, amepatikana na hatia katika mashtaka yanayojumuisha usaliti, mauaji, unyanyasaji wa kingono, mateso na uasi.

Kabila, ambaye aliitawala DRC kuanzia mwaka 2001 hadi 2019, aliondoka nchini humo mwaka 2023. Hata hivyo, mwezi Mei mwaka huu alionekana kwa muda mfupi katika maeneo ya mashariki ya nchi hiyo yanayodhibitiwa na waasi wa M23.

Kwa sasa haijulikani alipo baada ya hukumu hiyo ya mahakama ya kijeshi.

Kabila ambaye alimkabidhi madaraka mrithi wake Felix Tshisekedi kwa makubaliano, anamtuhumu kwa kupanga njama ya kummaliza kupitia kesi hiyo.

Mwendesha mashtaka alimshtaki Kabila kwa kuunga mkono waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, ambao mwaka huu wametwaa maeneo makubwa ya mashariki yenye utajiri wa madini. Kesi yake ilianza kusikilizwa bila ya yeye kuwepo tangu Julai.

Chanzo: DW Swahili

Related Posts