Nature

RASMI: Samia Suluhu Hassan Achukua Fomu ya Kugombea Urais

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amechukua fomu Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC Jijini Dodoma, leo Agosti 09, 2025.

Rais Dkt. Samia akiwa ameambatana na Mgombea mwenza Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekabidhiwa fomu hiyo na Mwenyekiti wa Tume uhuru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele

Wagombea hao watapeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Related Posts