
Droo ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imefanyika leo Februari 27, 2026 mjini Nyon, Uswisi huku Mabingwa wa kihistoria wa Ligi hiyo, Real Madrid wakipewa mfupa mgumu, Manchester City wakati Washika Mitutu, Arsenal wakipata mteremko baada ya kupangiwa Bayer Leverkusen.
Paris Saint Germain imepewa fursa ya kulipa kisasi dhidi ya Chelsea baada ya kuchezea kichapo kwenye fainali ya Kombe la Dunia la vilabu wakati Barcelona ikikutanishwa na Newcastle United ya England.
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu England, Liverpool watachuana na Galatasaray waliowaondosha Juventus kwenye ‘playoff’ huku Bayern Munich wakipewa mfupa uliomshinda Dortmund kwenye ‘playoffs’, Atalanta.
Njia ni nyeupe kwa Arsenal kufika fainali kwani ikiwa watapita mbele ya Leverkusen watakutana na mmoja Kati ya Sporting CP au Bodo/Glimt kwenye hatua inayofuata kabla ya kukutana Barcelona kwenye nusu fainali kama mambo yatakwenda vizuri kwa miamba hiyo ya Uhispania.
RATIBA KAMILI
Real Madrid 🇪🇸 Vs 🏴 Manchester City
PSG 🇫🇷 Vs 🏴 Chelsea
Bayer Leverkusen 🇩🇪 Vs 🏴 Arsenal
Galatasaray 🇹🇷 Vs 🏴 Liverpool Atalanta 🇮🇹 Vs 🇩🇪 Bayern Munich
Newcastle 🏴 Vs 🇪🇸 Barcelona
Atletico Madrid 🇪🇸 Vs 🏴 Tottenham
Bodo/Glimt 🇳🇴 Vs 🇵🇹Sporting
