
Habari za Leo ALKEBULAN ☀️
Thamani ya kipimo cha mia yetu na thamani ya mia yao tofauti zake ni nini?
Zamani kabla ya pesa watu walikua na mifumo tofauti ya kibiashara
- Mfumo wa kubadilishana mali- mfano mkulima anatoa nafaka anapata samaki kutoka kwa mvuvi
- Pesa za bidhaa- mfano chumvi, vitambaa, maganda ya kauri, mifugo na baadae metali za fedha na dhahabu
- Risiti za dhahabu- watu waligundua kuwa dhahabu na fedha(silver) zina uzito hivyo badala ya kubeba dhahabu halisi, walizihifadhi benki kwa ajili ya usalama na walipewa risiti. Walitumia hizo risiti kama njia ya malipo kwa ajili ya kununua bidhaa
- Baada ya risiti za dhahabu serikali ya Marekani iliamua kuondoa huo mfumo wa pesa kuthamanishwa na dhahabu mtu alizonano na kutambulisha pesa kuungwa mkono na amri ya serikali na imani ya watu na huu ndio mfumo unaotumima mpaka leo
Swali langu ni; Je, ina maana kwa sasa maneno ya mzungu na amri zake zina thamani zaidi ya dhahabu ya Muafrika….?
Inakuaje kwamba Afrika ndio inayozalisha madini (dhahabu,almasi,tanzanite n.k) ilhali pesa ya Muafrika haina thamani kama pesa ya mzungu? Dola unayoweza kuibeba kwenye pochi ukiibadilisha ikawa shilingi unabeba kwenye gunia 🥴
Nini kinafanya tunashindwa kulipinga hili wakati sisi ndio wenye madini yanayothamanisha haya makaratasi yanayotumika kama pesa?
Tupe maoni yako👇🏽

