Nature

Rose Ndauka Afunguka Mapya ya AJALI Mbaya Waliyoipata Wakielekea Tanga

Ahsanteni sana wapenzi wangu kwa mapenzi yenu makubwa sana mliyonionyesha na mnayoendelea kunionyesha….

Ahsante Mama yangu kipenzi @mamamawigi wewe kweli ni Mama..

Mnisamahe siwezi pokea simu zote ila kwa kifupi tumepata ajali saa 11,30 alfajir tukiwa tunatoka Dar kwenda Tanga, Hakuna aliyepoteza uhai japo wote tumepata majeraha na kunaendelea na tiba

Na kwa wale mnaoniomba niwekee namba kwa kunisupport mnaweza kutumia namba +255716995561 jina Rose Ndauka,..

Kwa atakayeona Pochi nyeusi Ina mistari stari Ina passport,hela pamoja na Simu Iphone 16….tunaomba atupigie kwa namba hiyo

Tunapenda kutoa Shukrani za dhati kwa wale Watanzania tusio wafahamu lakini wametusaidia na kuhakikisha tunapata msaada mbarikiwe sana

Bila Kusahau Askari police wa Michungwani waliotuokoa na kutupeleka Hospital…

Related Posts