Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUUMA), Salum Mwalimu leo August 12,2025 ameingia kwa mbwembwe katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) zilizopo Njedengwa, Jijini Dodoma, kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais.
Akiwa ameambatana na Mgombea mwenza wake, Mwalimu amewasili akiwa amesindikizwa na msafara mkubwa wa waendesha bodaboda waliokuwa wakipiga honi, kupeperusha bendera za Chama na kuimba nyimbo za kuhamasisha.

