Nature

Seleman Mwalimu Gomez ni Balaa, Anahitaji tu Muda na Nafasi Ndani ya Simba, Tanzania Itamuimba

Natamani Tanzania ingekuwa kama Uingereza namna ambavyo wamekuwa na moyo mkunjufu wa kuwasapoti wachezaji wao wa kizawa na kuwapa promo kubwa kuliko hata uwezo wa mchezaji

Ukweli ukimuangalia namna ambavyo anacheza Seleman Mwalimu hakuna mshambuliaji ndani ya Simbasc ambaye anafikia ubora ambao yuko nao

πŸ‘‰ Uwezo wa kucheza kwenye eneo kubwa la uwanja
πŸ‘‰ Uwezo mkubwa wa kunusa hatari
πŸ‘‰ Ubora kwenye kumalizia nafasi
πŸ‘‰ Uwezo wa kubadilisha nusu nafasi na kuwa nafasi kamili
πŸ‘‰ Kucheza namba zaidi ya moja 7,10,11,9
πŸ‘‰ Uwezo mzuri wa kutumia miguu yote miwili
πŸ‘‰ Aina yote ya mipira anaweza kufunga (kichwa na miguu)
πŸ‘‰Kasi na nguvu
πŸ‘‰ Beki wawili mpaka watatu sio kitu kwake

Ukiangalia kwa aina ya washambuliaji ambao wako kwenye kikosi cha simbasc utagundua mwalimu ni bora zaidi ya wote

Changamoto ya Mwalimu ni Utanzania wake ambao yuko nao wenda angekuwa anatoka nje ya mipaka ya Tanzania angepewa nafasi kubwa kwenye kikosi

Ukweli mara chache sana kwa miaka ya hivi karibuni timu zetu za simba na yanga kuamini mshambuliaji mzawa wa kati

Maana hata Yangasc wana Mzize lakini achezi kama namba 9 mara nyingi utokee pembeni mara chache ndiyo upata nafasi hiyo ya kucheza kati kwa zalula

Naamini kama Simbasc wakampatia vitu viwili kwa maana ya nafasi ya kucheza na muda wa kumvumilia basi watavuna matunda kwa kijana huyu wa kitanzania.

Related Posts