Serikali ya Uganda Yaagiza Kuzima Internet Mpaka Uchaguzi Umalizike

Mamlaka ya Mawasiliano ya Uganda imewaamuru watoa huduma za intaneti nchini humo kuzima huduma zao hadi itakapotangazwa tena.

Hatua hiyo inajiri wakati nchi hiyo ikielekea kwenye Uchaguzi wa Rais na Wabunge siku ya Alhamisi na inakuja baada ya kampeni kumalizika.

Katika barua iliyotolewa kwa Vyombo vya habari vya ndani, wakala wa Serikali iliwaandikia watoa huduma za mtandao, kuwataka kusubiri hadi taarifa zaidi kabla ya kurejesha huduma za mtandao.

Wiki iliyopita Mpinzani mkubwa wa Rais Yoweri Museveni, Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine alikuwa wa kwanza kutangaza kwamba Serikali ilipanga kuzima Mtandao wakati wa Uchaguzi, kama ilivyofanya wakati wa Uchaguzi wa 2021.

Wapinzani wanasema kwamba kuzimwa kwa mtandao kwa sasa ni jaribio la kufanya kazi mahali penye giza ambapo hakuna habari huru kuhusu maudhui yanayowafikia wananchi, isipokuwa yale yanayodhibitiwa na Serikali kupitia vyombo vyake vya habari.

Related Posts