Uongozi wa Simba umefanya maamuzi ya kumfuta Kazi Meneja Kivuli ambaye ukweli wa mambo ndiye aliyekuwa Kocha mkuu baada ya kuondoka Fadlu
Matokeo mabaya ambayo Simba imeyapata hapa karibuni hayana uhusiano wa moja kwa moja na Kocha ni muendelezo wa kuishi kwa mazoea na kujiongopea yanapotokea magumu , ukiniuliza mimi nitakwambia shida ya Simba SC wala sio Kocha
Shida ya Simba ni kutokuelewana kwa viongozi wa juu ambao mvutano wao unashuka hadi chini na kuathiri utendaji wa wachezaji , kwa hali ya Simba ilivyo sasa wanaweza kumuachia timu Matola bado asiwafikishe nchi ya ahadi walichofanya leo ni kuhamisha mjadala ili watu waache kujadili ubovu wa uongozi wajadili kuondoka kwa kocha [ Inaitwa Funika Kombe ]

