Msanii na mfanyabiashara maarufu nchini, Zena Mohamed @officialshilole leo Juni 29, 2025, amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) katika Mkoa wa Tabora.
Shilole alipokelewa rasmi katika Ofisi za CCM Mkoa wa Tabora na Katibu wa UWT mkoa huo, Rhoda John Madaha, wakati wa kukabidhiwa fomu hiyo ya kugombea.
Hatua hiyo inamuweka Shilole kwenye orodha ya wanawake mashuhuri wanaoingia kwenye siasa za uwakilishi bungeni kupitia UWT, baada ya kujipatia umaarufu mkubwa kupitia sanaa ya muziki na biashara.
Uamuzi wake unakuja katika kipindi ambacho wanawake wengi wameanza kujitokeza kuchukua nafasi za uongozi wa kisiasa nchini, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha usawa wa kijinsia na ushiriki wa wanawake katika maamuzi.

