Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa adhabu kali kwa Senegal na Morocco

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa adhabu kali kwa Senegal na Morocco kufuatia vurugu wakati wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025.

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Senegal Pape Bouna Thiaw ametozwa faini ya USD 100,000 (TSh. Milioni 255,500,000), baada ya kuwaamuru wachezaji kutoka Uwanjani.

Kwa upande wa Wachezaji, Iliman Cheikh Baroy Ndiaye na Ismaila Sarr wamefungiwa kila mmoja mechi mbili rasmi za CAF kwa tabia mbaya dhidi ya Mwamuzi.

CAF imelitoza shirikisho la Senegal faini ya dola 300,000 (TSh. Milioni 768,000,000) kwa utovu wa nidhamu wa mashabiki wake na Dola nyingine 300,000 kwa tabia ya utovu wa nidhamu kwa wachezaji wake na wafanyakazi wa kiufundi.

Kwa upande wa Morocco beki nyota Achraf Hakimi amefungiwa kucheza mechi mbili rasmi za CAF.
Morocco imetozwa faini ya Dola 200,000 (TSh.Milioni 511,000,000)kwa tabia isiyofaa ya wachezaji wa mpira uwanjani wakati wa fainali, huku faini ya Dola 100,000 ikitozwa kwa utovu wa nidhamu wa wachezaji wa Morocco na wafanyakazi wa kiufundi, ambao walivamia eneo la ukaguzi wa VAR na kuzuia kazi ya Mwamuzi.

Related Posts