✍🏼 Simba walianza game vizuri sana , wakiwa na mpira wanaconnect pass zao vizuri na bila umiliki wanakuwa na muundo mzuri wa kuzuia …. Kivipi ?
1: Simba wakiwa na mpira wanaunganisha pass zao vizuri kutokea nyuma , Kante na Kagoma wanakuwa karibu na CBs wao then mawinga wao wanakuwa zaidi kuwaruhusu FBs kufanya Underlaping kushambulia half spaces .
2: Dhumuni ni kupata nafasi eneo la ndani na nyuma ya kiungo cha Esperance ambao walikuwa wanazuia kwenye muundo wa 4-4-2 tena wakiwa karibu karibu sana … Baada ya hapo ni ?
3: Simba watakuwa na uharaka kwenye maamuzi , runner kwa wachezaji wa mbele + usahihi wa pass zao : Nafikiri kama dakika 15 za mwisho kipindi cha kwanza walifanya vitu kwa ubora mkubwa hasa wakati wanashambulia ( Baada ya hapo wakaonesha ukatili kwenye nafasi zao “ PERFECT “ .
✍🏼 Kipindi cha pili , Nafikiri baada ya Kagoma na Kante kutoka ndio Esperance walipopata nafasi nyuma ya kiungo cha Simba , viungo wao wakaanza kutengeneza overload eneo la ndani , wakawa wanapata nafasi eneo la ndani rahisi kufika eneo la mwisho .
✍🏼 Baada ya hapo nafasi zikawa zinafunguka tu kwa upande wao .
NOTE :
1: Kante pass kwenda kwa Oura then movement ya Kibabage + Position ya Kapombe 🔥” PERFECT “ .
2: Oura na Gueye wameongeza kitu kikubwa sana kwa Simba : Kasi , Utulivu + ufundi ( ngumu kubaliana nao kwenye 1 vs 1 )
3: Kante ubora wa pass zake za mbele 🔥
4: Msakni na Jebali wakiwa na mpira ngumu kuchukua mali ( Ufundi , dribbler then ni passer wazuri 🙌 ) .
5: Ile kamba ya Boualia “ CLASSY “ 🙌 Danho kacheza game nzuri .
6: SIMBA KIPINDI CHA PILI WALIKUWA WAZI SANA .
FT : Simba 2-2 Esperance
