Anaandika @kelvinrabson_
✍🏼 Nafikiri plan ya kocha wa Simba “Diminter Pantev” kuanza bila mshambuliaji haikuwa sahihi kwa muda mwingi kiwanjani walikosa uhatari kwenye eneo la juu . Walikuwa slow sana kwenye maamuzi yao , walishindwa mipambano yao dhidi ya defense ya Petro hata build up yao kuanzia chini nayo haikufanikiwa kwanini ?
1: Wakati wanaanza build up kama kawaida kiungo mmoja anashuka chini kutengeneza Back 3 ( De Reuck – Nangu – Kante ) baada ya hapo walikosa machaguo ya pass zao hasa kupitia ndani .
2: Ni kwasababu Petro walikuwa na idadi nzuri ya wachezaji kwenye kiungo na walifika kwenye matukio kwa wakati sahihi rahisi kwao kutibu mipango ya Simba wakati wanaanza mpira nyuma , plan yao ikawa kutumia mipira mirefu “Long balls” kushambulia nafasi nyuma ya defense ya Petro .
3: Petro walionekana kuzuia kwenye high line ( walinzi wao wanakuwa karibu na mstari wa kati ) faida yake ni kuwanyima Simba uhuru wa kuanzia mpira nyuma baada ya hapo Simba waliamua kutumia mipira mirefu nyuma ya defense ya Petro , plan ilikuwa sahihi lakini utekelezaji wa wachezaji wa mbele ndio uliwaangusha ( kuna nafasi nzuri walipata ila Ufanisi ulikuwa mdogo )
✍🏼 Kipindi cha pili : Petro walibadilika sana tofauti na kipindi cha kwanza …. Kivipi ?
1: Waliongeza kasi kwenye maamuzi yao pale wanapokuwa na mpira ( fanya mpira utembee haraka na kwenye nafasi )
2: Walishinda mipambano yao vizuri na zile second balls .
3: Bila mpira wanakuwa na idadi nzuri ya wachezaji kwenye kuzuia + wakiwa na mpira wanakuwa karibu karibu sana rahisi kwao kuunganisha pasi kufika eneo la mbele .
NOTE :
1: Nafikiri plan ya Simba kuanza na false 9 iliwanyima idadi nzuri ya wachezaji kwenye box la mpinzani .
2: Gigal kacheza game nzuri sana : kasi , ufundi + kujiamini 🔥
3: Jonathan Toro anafanya kazi yake vizuri sana na mpira mguuni .
4: Kante analinda vizuri nafasi ( Utulivu , pass zake kwenda mbele na mzuri kwenye kushinda duels zake )
5: Gilberto kwenye 1 vs 1 ngumu kukabiliana nae .
6: Huwezi kuwa unakosa nafasi za wazi kama vile tena level ya kimataifa na utegemee matokeo chanya kirahisi . ( Simba wamekosa nafasi nzuri mno )
FT : Simba 0-1 Petro Atletico
View all 121 comments

