Mlinzi wa pembeni Nickson Kibabage amejiunga na Simba Sports Club akitokea Singida Black Stars, Kibabage amejiunga na Simba kwa mkataba wa Mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine
Kibabage ni Moja ya mabeki wazawa mwenye uwezo Mkubwa wa kushambulia na kuzuia huku akiwa na uzoefu wa kutosha kwenye ligi kuu na michuano ya kimataifa
Aidha Kibabage alikuwa miongoni mwa wachezaji walioiwakilisha Tanzania kwenye AFCON 2025 nchini Morocco ambapo Tanzania ilifika hatua ya 16 Bora kwa mara ya kwanza.
