Simba Wanaingia Kwenye Derby Wakiwa Wanyonge

Zikiwa zimesalia siku 2 na masaa kadhaa kabla ya Derby ya Kariakoo kupigwa visiwani Zanzibar

▫️Yanga SC wanaingia wakiwa na rekodi ya kutawala mchezo huo kwa siku za karibuni wakishinda mfululizo.

▫️Yanga SC pia wanaingia kwenye mchezo huo bila presha kwani wapo kileleni kwa tofauti ya alama 5 vs Simba SC lakini pia wameshinda mechi zote 5 za mwisho za Ligi kuu

▫️Simba SC wanaingia kwenye Derby wakiwa wanyonge na hii ni kutokana na rekodi mbaya ya kufungwa mfululizo kwenye mechi za derby miaka ya karibuni.

▫️Simba SC pia Wanaingia wakiwa na unyonge wa kudondosha alama 2 hapo jana zinazowafanya wawe nyuma kwa alama 5 na safari yao ya ubingwa kuwa na mawimbi mengi.

Hivi ndivyo ambavyo wote wanaingia , Je watatokaje ____

Related Posts