Mohammed Omar Ali Bajaber amefunga bao lake la kwanza ndani ya uzi wa Simba Sc kwenye mechi ya kiushindani kwenye mguso wake wa kwanza ‘First Touch’ na kuisaidia Simba Sc kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya ‘Purple Nation’ Mbeya City katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Dar es Salaam.
Simba Sc imefikisha alama 12 baada ya mechi nne na kukwea mpaka nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara, alama moja nyuma ya Yanga Sc iliyopo nafasi ya tatu (Yanga wamecheza mechi moja zaidi)
FT: Simba Sc 3-0 Mbeya City.
⚽ 28’ Morice
⚽ 38’ Sowah
⚽ 85’ Bajaber
🟥 23’ Mayanga

