Singida Black Stars Watamba na Sowah “Kama Una Bilioni 2.6 Njoo Uongee”
Last updated Jul 25, 2025
Share
Klabu ya Singida Black Stars imetoa kauli ya kusisimua kuhusu mshambuliaji wao tegemeo, Jonathan Sowah, wakisisitiza kuwa hakuna timu yoyote ndani ya Tanzania yenye uwezo wa kifedha wa kumsajili mchezaji huyo.
Kupitia kwa Afisa Habari wa klabu hiyo, Husein Massanza, Singida Black Stars imesema kuwa klabu yoyote inayotamani huduma ya Sowah itatakiwa kuweka kitita cha Dola za Kimarekani milioni 1, sawa na takriban Shilingi bilioni 2.6 za Kitanzania, mezani.
“Ikitokea klabu inakuja inataka kumnunua Jonathan Sowah, inaona inajiweza – weza. Dau mezani ni dola milioni 1. Tunathubutu na kujiamini tukisema kwamba kwa Tanzania hakuna klabu yenye uwezo wa kutoa bilioni 2.6,” amesema Massanza.

