Nature
Aziz K na Hamisa Mobetto

SIRI Yafichuka Kilichomdatisha Aziz K Kwa Hamisa Mobeto Hichi Hapa

Mwanamitindo Hamisa Mobeto amesema linapokuja suala la kuvaa kwake huwa hana mpinzani kwani hataki mchezo kwenye sekta hiyo na ni moja ya vilivyomdatisha mumewe Stephanie Aziz Ki kumpenda.

Hamisa aliliambia Mwanaspoti ana chumba kizima kwa ajili ya nguo na viatu tu pamoja na maendeleo anayoyafanya katika maisha yake, lakini suala la mavazi humchukulia sehemu kubwa ya pesa zake kwani ana viatu vingi na nguo ambazo hata wakati mwingine hakumbuki kuzivaa.

Alisema hata mume wake Aziz KI kitu kimoja kwake alichompendea ni kuvaa vizuri na kupendeza.

“Kiukweli ninajipenda sana linapokuja suala la kuvaa na kuonekana mrembo huwa natumia pesa nyingi, yaani nina chumba maalumu kwa ajili ya ishu ya mavazi tu. Humo utakuta kila aina ya nguo na aina ya viatu pamoja na ‘dressing table’ ya kujifanyia ‘make up’.

“Pia huku kuvaa kwangu mume wangu Aziz KI huwa anapenda sana kuona napendekeza na ndiyo sababu moja wapo ya kunipenda japo zipo nyingi ni siri yangu,” alisema Hamisa.

Aziz K na Hamisa Mobeto

Related Posts