Sugu Aishauri Serikali Bei ya Mafuta Tanzania

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’
Picha: Mpigapicha Wetu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameishauri Serikali kuondoa kodi ya kwenye mafuta ili nishati hiyo ishuke na kuwapunguzia mzigo wananchi.

Sugu ameyasema hayo alipozungumza na Nipashe Digital kuhusu madhara ya kupanda kwa bei ya nishati hiyo ambayo imesababisha mgomo wa magari ya abiria kwenye baadhi ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

Ameema zaidi ya nusu ya bei ya mafuta nchini huwa ni kodi za serikali ambazo amedai huwa zinalipwa na wananchi na hivyo akaishauri serikali kuondoa kodi hizo ama kuzipunguza kama ambavyo baadhi ya mataifa yamefanya.

“Afrika Kusini na baadhi ya mataifa duniani yameondoa kodi za mafuta ili kudhibiti mfumuko wa bei za vitu ndani ya nchi zao, bei ya mafuta inapokuwa kubwa hata gharama za vitu vingine ikiwemo vyakula hupanda na nauli zinapanda hali ambayo inakuwa maumivu kwa wananchi,” amesema Sugu.

Amesema kutokana na tatizo hilo hata baadhi ya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakitumia vyombo binafsi vya usafiri wanashindwa kuvitumia kwa sababu ya gharama kubwa ya mafuta.

Related Posts