Taarifa Kuhusu Victor Osimhen Kujitoa Timu ya Taifa ya Nigeria Kisa Mchezaji Lookman

Ripoti zilizothibitishwa sasa zinasema kuwa mshambuliaji nyota Victor Osimhen ametangaza wazi kuwa amemalizana na timu ya taifa ya Nigeria. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Osimhen aliacha kitambulisho chake cha mashindano (accreditation) na kusema kuwa anarudi nchini Uturuki.

Taarifa hiyo imeripotiwa na OneJoblessBoy kupitia mtangazaji wa Arise TV, Aron Akerejola.

Hatua hiyo imezua mshtuko mkubwa ndani ya kambi ya Super Eagles na miongoni mwa mashabiki wa soka barani Afrika, hasa ikizingatiwa kuwa Nigeria ipo katikati ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Hadi sasa, Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) halijatoa tamko rasmi kufafanua tukio hilo, huku sintofahamu ikiendelea kuongezeka kuhusu mustakabali wa timu hiyo katika mashindano yanayoendelea.

Hivi karibuni kumeibuka taarifa mitandaoni zikidai kuwa mshambuliaji nyota wa Super Eagles victor Osimhen ameamua kuacha timu ya taifa ya Nigeria katikati ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) Taarifa hizo zilidai kuwa Osimhen aliacha kitambulisho chake cha mashindano (accreditation) na kueleza nia ya kurejea nchini Uturuki ambako anachezea klabu yake.

Kwa mujibu wa ripoti zilizosambazwa kupitia akaunti ya #OneJoblessBoy kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) zikimnukuu mtangazaji wa Arise TV Aron Akerejola hatua hiyo inadaiwa ilifuata mvutano wa uwanjani kati ya Osimhen na mwenzake Ademola Lookman hali iliyoibua sintofahamu kubwa miongoni mwa mashabiki.

Hata hivyo Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) limekanusha vikali madai hayo likisisitiza kuwa Osimhen hajaondoka kambini wala hajatangaza nia ya kuacha timu ya taifa NFF imesema mvutano wowote uliotokea umeisha kutatuliwa ndani ya timu na hali kambini ipo shwari.

Mpaka sasa hakuna tamko rasmi kutoka kwa Victor Osimhen mwenyewe kuhusu suala hilo huku NFF ikisisitiza kuwa timu inaendelea na maandalizi ya mechi zijazo za AFCON Hivyo taarifa za kuondoka kwake zinaendelea kuchukuliwa kama uvumi unaosambaa mitandaoni.

Related Posts