Klabu ya Wydad AC imethibitisha kuwa mchezaji wake, Stephen Aziz Ki, yuko salama na anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa masaa 24, kama ilivyopendekezwa na ushauri wa madaktari, kutokana na jeraha la kichwa alilopata usiku wa jana katika mechi dhidi ya Azam FC.
Aziz Ki alipata majeraha hayo dakika ya 77 ya mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika, ambapo timu yake ilishinda bao 1-0 dhidi ya Azam FC, na mara moja alihitajika kusafirishwa hospitalini.
Taarifa ya klabu imeeleza kuwa mchezaji huyo atabaki chini ya uangalizi maalum wa masaa 24, na mabadiliko yoyote katika hali yake yatafahamishwa mara itakapobainika.

