DIPLOMASIA: Kufuatia tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kutaka nchi 36 (ikiwemo Tanzania) kufanyia kazi baadhi ya mambo ya kiuhamiaji ambayo yanaweza kusababisha raia kuzuiwa kuingia Marekani, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali ya Tanzania imeanza mashauriano
Amesema, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, imeanza kufanya mashauriano na wenzao upande wa Marekani kujua maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa maboresho, hususani yanayohusiana na masuala ya kikonselii ili kuharakisha Tanzania isiwe moja ya nchi zitakazozuiwa kuingia Marekani
Tamko la Serikali linakuja baada ya Donald Trump kutaka nchi 36 kufuatilia na kutoa taarifa kabla ya Julai 18, 2025, kuhusu utayari wa nchi zao kuboresha hati za usafiri kwa raia wao, pamoja na kuchukua hatua kuhusu raia wao walioko Marekani kinyume cha sheria

