Siku ya Jumapili September 30 klabu ya Simba itakuwa ni kikao maalumu cha Wanachama katika ukumbi wa Diamond Jubilee Kuanzia majira ya saa 2 Asubuhi. Simba inakwenda kufanya kikao chake kwa mujibu wa katiba yake lakini nyuma ya Pazia Kuna makubwa na mazito Zaidi ambazo pengine Wadau wengi wa klabu Hawajui.
Kwa mujibu wa Hans Rafael ni kua wale wale DP World ambao wanatajwa kuchukua uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam wako kwneye hatua za awali kabisa Kwa ajili ya kuchukua Simba na kua wawekezaji rasmi huku Mo Dewji akitoka nje.
Serikali Inapigilia Msumari
Pia mwandishi Nassib Mkomwa ameweza kuweka baadhi ya matakwa ya serikali ambayo inataka Simba kufanyia kazi mara Moja na haraka Tena katika kikao hicho cha Jumapili hii. Serikali inataka kwanza kufanyika tathmini Upya ya thamani halisi ya klabu ya Simba.
Pili serikali inataka mali zote ambazo hazihamishiki kama Majengo ya Simba kua chini ya asilimia 51 ambazo ni hisa za Wanachama wa klabu ya Simba. Huku asilimia 49 za muwekezaji ( Mo Dewji ) kuendelea kua chini yake wakati tathmini ya Logo ya timu inaendelea Kupigwa hesabu Upya.
DP World inatajwa kuja na mpango mpya wa kuweza kuchukua klabu ya Simba huku kampuni hiyo ya falme za kiarabu ikiendelea kutanua wigo wake mkubwa na mpana kwa ajili ya uwekezaji wa Kibiashara Afrika na Duniani kwa ujumla.

