
TFF imethibitisha kuwa mchezaji huyo ni mwanamke halali baada ya kupitia vipimo vyote vya kitabibu vilivyofanywa kwa ushirikiano na wataalamu wa afya Kufuatia matokeo hayo shirikisho limefuta zuio la awali lililomnyima kushiriki michezo ya timu hiyo
Kupitia barua rasmi iliyoifikia klabu ya Yanga Sc TFF imeruhusu rasmi Jeanine Mukandiyisenga kurejea uwanjani na kushiriki kwenye mechi ijayo ya timu hiyo

