
Staa wa muziki kutokea Nigeria, Tiwa Savage, 45, amesema yupo tayari kuolewa mke wa pili kwa sababu umri wake umeshaenda sana!.
Utakumbuka Tiwa Savage, mkali wa kibao, Kele Kele (2013), kwa sasa ni mama wa mtoto mmojq, Jamil Balogun aliyempata katika ndoa yake iliyovunjika.
“Wanaume wanaonifaa kwa sasa wako kwenye miaka 50 huko au wameshaoa. Na kweli hao ndio wamekomaa. Mimi nitachojali ni kuishi vizuri na mke wa kwanza” amesema.
Ikumbukwe akiwa na miaka 11, Savage alihamia London, Uingereza kwa ajili ya masomo, miaka mitano baadaye alianza kazi yake ya muziki akiimba nyimbo za wasanii kama vile George Michael na Mary J. Blige hadi alipokuja kuhitimu chuo cha muziki cha Berklee.
Mwaka 2012 alirejea Nigeria na kusaini Mavin Records inayomilikiwa na Don Jazzy na mwaka uliofuatia alitoa albamu yake ya kwanza, Once Upon a Time (2013) ikiwa na nyimbo kama ‘Kele Kele Love’ ambao ulivuma sana Afrika na kumtambulisha vizuri
