TMA Yatoa Tahadhari ya Mvua Kubwa Mikoa 20

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa katika maeneo ya mikoa 20 nchini.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na TMA siku ya Jumamosi, tarehe 27 Desemba 2025, mikoa itakayoadhirika ni Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Morogoro, Ruvuma, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani, ikijumuisha pia Kisiwa cha Mafia.

TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuanzia Jumapili, tarehe 28 Desemba 2025, na zinaweza kusababisha mafuriko, maporomoko ya ardhi, pamoja na usumbufu katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Wananchi wa maeneo husika, hususan wanaoishi kwenye mabonde na maeneo hatarishi, wanahimizwa kuchukua tahadhari zote muhimu ili kujilinda na madhara yanayoweza kutokea.

Aidha, mamlaka imewataka wananchi kufuatilia taarifa za hali ya hewa mara kwa mara ili kupata taarifa sahihi na za wakati.

Related Posts