TMA Yatoa Utabiri Hali ya Hewa Siku 10 Zijazo

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa mwenendo wa mvua kwa kipindi cha tarehe 11 hadi 20 Desemba 2025, ikionyesha kuendelea kwa hali ya mvua katika maeneo mbalimbali nchini..

Kwa mujibu wa TMA, mifumo ya hali ya hewa inaonyesha kuimarika kwa migandamizo mikubwa ya hewa katika maeneo ya kaskazini mwa dunia (Azore na Siberia), huku ile ya kusini (St. Helena
na Mascarene) ikiendelea kudhoofika. Mabadiliko haya yanatarajiwa kusababisha ukanda wa ukandamvua (ITCZ) kusogea zaidi kusini na kuwepo katika maeneo ya Ziwa Victoria, magharibi, kati na kusini mwa nchi. Hali hii itaongeza uwezekano wa mvua katika maeneo hayo.

Aidha, upepo wenye unyevunyevu uvumao kutoka baharini kuelekea ukanda wa pwani unatarajiwa kuimarisha mifumo ya mvua katika maeneo hayo..

Mwelekeo wa mvua Kuanzia Desemba 11-20, 2025

Kanda ya Ziwa Victoria (Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache.

Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki (Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Mvua zinatarajiwa katika maeneo machache.

Pwani ya Kaskazini (Tanga, kaskazini mwa Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Unguja na Pemba):
Mvua katika maeneo machache zinatarajiwa.

Magharibi mwa Nchi (Kigoma, Katavi na Tabora):
vua na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache.

Kanda ya Kati (Dodoma na Singida): Mvua zinatarajiwa katika maeneo machache.

Nyanda za Juu Kusini Magharibi (Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Mvua zinazoambatana na ngurumo zinatarajiwa katika maeneo machache.

Pwani ya Kusini (Mtwara na Lindi): Mvua zinatarajiwa katika maeneo machache.

Kanda ya Kusini (Ruvuma na kusini mwa Morogoro):
Mvua zinatarajiwa katika maeneo machache.

Related Posts