
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Wakili Tundu Lissu imeendelea tena leo.
Akiwa Mahakamani hapo, Lissu amelieleza jopo la Majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo likiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru kuwa ametuma barua hiyo tangu Septemba 04.2025 lakini hadi sasa barua hiyo hajajibiwa
“Niliandika barua kwa Msajili nikiomba kesi hii irushwe ‘live’ kwa sababu ni kesi kubwa lakini mpaka sasa sijajibiwa, naomba kesi hii irushwe ‘live’ kwa sababu ya ukubwa wake, ni hayo tu Waheshimiwa Majaji” -Lissu
Inaelezwa Baada ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo Mahakamani hapo, upande wa jopo la Mawakili wa Jamhuri/ Serikali ukiongowa na Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga umekiri kupokea nakala (copy) ya barua hiyo (barua ya Tundu Lissu iliyotumwa kwa Msajili wa Mahakama) lakini hata hivyo amesema jambo hilo wanaiachia Mahakama ifanye maamuzi yake kwani hilo liko kwenye maamuzi yake
Hata hivyo, Jamhuri imesisitiza kuwa katika maamuzi yake Mahakama inapaswa kuzingatia kuwa (kama ‘live’ itakubaliwa) basi inapaswa kufanyika wakati kesi ya msingi itakapoanza kusikilizwa
“Waheshimiwa Majaji kuhusu hili ombi, sisi tunakiri kupewa nakala (copy) ya kuomba ‘live streaming’ lakini ni Mahakama hii ndio ina mamalaka ya kuamua juu ya hili, Waheshimiwa Majaji hili ni ombi linatakiwa lifanywe wakati kesi inapoanza kusikilizwa ‘trial’ na kwa sasa bado hatujaanza ‘trial’ sitaki kurudia maneno ambayo Mahakama imeshaamua, kwakuwa sasa haymtuko kwenye ‘commital’ wala kwenye ‘trial’ ni maombi yetu kuwa asubiri wakati mwafaka tutakapokuwa kwenye ‘trial’ wakati ambao atakuwa ameshasomewa mashtaka ila sio kwasasa” -Wakili Katuga
