Ujenzi Uwanja Mpya wa Mpira Arusha Wafikia Pazuri

Uwanja wa Arusha umefikia hatua ya asilimia 74 ya ujenzi, ikiwa ni maandalizi muhimu kuelekea Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 yatakayofanyika kwa pamoja nchini Tanzania, Kenya na Uganda. Uwanja huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 2026 na kuwa miongoni mwa viwanja vitakavyotumika rasmi katika mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika.

Ujenzi wa uwanja huo unaendelea kwa kasi, ambapo tayari miundombinu ya msingi ikiwemo majukwaa ya watazamaji, sehemu za wachezaji na mifumo ya huduma muhimu imeanza kuonekana katika hatua za mwisho. Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imekuwa ikisisitiza kukamilika kwa mradi huo kwa wakati ili kuendana na viwango vya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Kukamilika kwa Uwanja wa Arusha kunatarajiwa kuupa mkoa huo fursa ya kiuchumi na kijamii, ikiwemo kukuza utalii, biashara na ajira kwa wakazi wa eneo hilo. Aidha, uwanja huo utaendelea kutumika kwa mashindano ya kitaifa na kimataifa hata baada ya AFCON 2027, hivyo kuimarisha hadhi ya Tanzania katika ramani ya michezo barani Afrika.

Related Posts