Wakati mashabiki wa Simba wakionyesha wasiwasi kuhusu kiwango cha kiungo mshambuliaji Elie Mpanzu. Kocha Steve Barker amemaliza utata huo akithibitisha kuwa Mpanzu yupo vizuri na hana tatizo lolote la kiufundi.
Barker amesema Mpanzu ni mchezaji muhimu sana katika utekelezaji wa falsafa ya timu, akisaidia hasa pale Simba inapopoteza mpira. “Ana juhudi kubwa uwanjani, anatupa nafasi za kufunga na kuunda mashambulizi, ingawa si lazima afungue au kuasisti kila mechi,” Barker aliongeza.
Kocha pia amewashauri mashabiki kumpa nguvu, akisema ukame wa mabao ni jambo la kawaida kwa wachezaji wakubwa. Mpanzu alifunga bao la mwisho Januari 18, 2026, dhidi ya Mtibwa Sugar, na ndiye miongoni mwa wachezaji wenye asisti nyingi kwenye timu.
Mashabiki watulie, Simba SC bado ina mechi nyingi, na Mpanzu atawapa furaha uwanjani.
