Nature

Umoja wa Nchi za Ulaya Watoa Tamko: Tumehuzunishwa na Vifo Tanzania, Familia Zipewe Miili

Umoja wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania kwa pamoja na Mataifa ya Uingereza, Canada, umetoa wito kwa Serikali ya Tanzania kutekeleza ahadi zake za kimataifa za kulinda haki za msingi ikiwemo haki za kikatiba za kupata taarifa na uhuru wa kujieleza kwa Watanzania wote.

Hayo yameeleza kupitia tamko la pamoja lililotolewa na Umoja wa Nchi za Ulaya hii leo Disemba 05, 2025 likirejelea tamko la Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya na tamko la pamoja la Mawaziri wa Mambo ya nje wa Canada, Norway Na Uingereza lililotolewa Octoba 31 2025 kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 ambapo tamko hilo limeeleza kuwa Umoja huo wa Ulaya umehuzunishwa na vifo na majeruhi wengi waliotokana na matukio ya Uchaguzi Mkuu.

Katika taarifa yake, Umoja huo pia umeeleza kuwa zipo taarifa za kuaminika kutoka Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa zimeonesha ushahidi wa mauaji nje ya utaratibu wa kisheria, kupotea kwa Watu, ukamataji wa Watu kiholela pamoja na kuwepo kwa ufichaji wa miili ya waliopoteza maisha hivyo umetoa wito wito kwa Mamlaka kukabidhi miili ya marehemu kwa familia zao, kuwaachia huru Wafungwa wote wa kisiasa na kuhakikisha waliokamatwa wanapata misaada ya kisheria na matibabu.

Kwa upande mwingine Umoja huo umetoa wito kwa Serikali ya Tanzania kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti ya awali ya Waangalizi wa Uchaguzi wa AU na SADC zilizoweka bayana mapungufu yaliyojiri wakati wa Uchaguzi “Tunakaribisha hatua ya Serikali ya kutambua kwamba kuelewa kiini na mazingira yaliyopelekea vurugu ikiwemo vifo ni hatua muhimu kuelekea upatikanaji wa haki na maridhiano, uchunguzi wowote ni lazima uwe huru, wazi na shirikishi ukijumuisha asasi za kiraia, Taasisi za kidini na Wadau wote wa kisiasa.

Millard ayo

Related Posts