Nature

Unaambiwa Kumbe Mama Fei Toto Kawafukuza Yanga…Kisa


Taarifa za kuaminika kutoka chanzo cha karibu na familia ya kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Feisal Salum “Feitoto”, zinaeleza kuwa mama mzazi wa mchezaji huyo amekataa kabisa kushiriki mazungumzo yoyote yanayohusiana na uhamisho wa mwanawe kurejea Yanga SC.

Inadaiwa kuwa Yanga imekuwa ikijaribu kwa njia mbalimbali kumshawishi Feitoto kurudi Jangwani, huku wakituma viongozi mbalimbali kwenda nyumbani kwao kumwomba msamaha kwa niaba ya wanachama na viongozi waliowahi kumkashifu hadharani. Hata hivyo, mama mzazi wa Feitoto amekuwa mkali na amewafukuza baadhi ya wajumbe waliowasili kwa mazungumzo hayo, akisema hataki hata kusikia jina la Yanga.

Chanzo hicho kinasema msimamo huo umetokana na kile kilichoonekana kuwa ni dharau alizotendewa mwanae na baadhi ya wanachama na viongozi wa Yanga akiwemo msemaji wa klabu hiyo kipindi Feitoto alipoamua kuondoka Jangwani na kujiunga Azam FC.

Kwa sasa, taarifa za ndani kutoka kwenye kambi ya wawakilishi wa Feitoto zinaeleza kuwa nyota huyo ameshafikia makubaliano na klabu kubwa zaidi Afrika Mashariki kwa sasa Simba SC, ambayo pia inashikilia nafasi ya tano kwa ubora barani Afrika kulingana na viwango vya CAF.

Ujio wa Feitoto Simba unaonekana kuwa pigo kubwa kwa Yanga, ambao walikuwa na matumaini makubwa ya kumrudisha mchezaji huyo kwa msimu ujao. Mashabiki wengi wa soka wanatazamia kwa hamu kutangazwa rasmi kwa usajili huo unaoweza kuongeza moto mkubwa kwenye kikosi cha Simba SC

Related Posts