
Israel imetangaza kuwa imeanza rasmi kuishambulia Iran katika maeneo kadhaa huku ikisema kuwa inachikifanya sasa ni mashambulizi ya tahadhari
Katika taarifa yake asubuhi ya leo Jumamosi, Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz ametangaza hali maalum na ya dharura kote Israel.
Milipuko mitatu imesikika katikati mwa jiji la Tehran, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran.
Shirika la Habari la Fars linasema kuwa limepokea taarifa kwamba makombora kadhaa yamepiga eneo mji mkuu wa Iran.
Walioshuhudia mjini Tehran wameiambia ABC News kwamba walisikia milipuko miwili katika mji mkuu wa Iran.
Haya yanajiri huku mvutano kati ya Marekani na Iran ukizidi kushika kasi kufuatia msururu mkubwa wa kijeshi wa Marekani katika Mashariki ya Kati na mazungumzo yanayoendelea kati ya Marekani na Iran kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yisrael Katz alitia saini agizo maalum la kutaka hali ya hatari kuwekwa nchini kote Israel.
“Lazima utii maagizo ya Kamandi ya Nyumbani na mamlaka na kubaki katika maeneo yaliyohifadhiwa,” ilisomeka taarifa hiyo
