Rais wa Uganda Yoweri Museveni atawania kuchaguliwa tena katika Uchaguzi wa Januari 2026.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 anatazamiwa kuchukua Fomu za uteuzi Jumamosi hii , akilenga kutetea nafasi yake kama Mwenyekiti wa Chama Tawala (NRM ) na kupeperusha bendera ya Chama hicho kwenye Uchaguzi ujao wa Mwakani.
Uchaguzi wa Januari 2026 utashuhudia Waganda wakimpigia kura Rais na Wabunge. Museveni ameiongoza Uganda tangu 1986.

