Wachezaji wa klabu ya Simba Sc, Jonathan Sowah na Allasane Kante wamefungiwa michezo mitano (5) na kutozwa faini ya Tsh. Milioni moja kila mmoja kwa kufanya vitendo visivyo vya kiuanamichezo kwenye kipigo cha Simba Sc cha 2-0 dhidi ya Azam Fc katika dimba la Benjamin Mkapa.
Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ambapo mshambuliaji Sowah ameadhibiwa kwa kosa la kumpiga kiwiko kiungo wa Azam Fc, Himid Mao huku kiungo Allasane Kante akiadhibiwa kwa kosa la kumpiga teke kwa makusudi kiungo Feisal Salum.
Katika hatua nyingine Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya ya TPLB imemfungia kiungo wa Singida Black Stars, Khalid Aucho michezo mitano na faini ya Tsh. milioni moja kwa kosa la kumpiga na kumsukuma mchezaji wa TRA United, Adam Adam wakati wa mechi kati ya timu hizo iliyomalizika kwa Singida Black Stars kulala 3-1.
