Katika kuadhimisha Miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo Desemba 9, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa elfu moja na thelathini na sita (1,036)
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. George Simbachawene imeeleza kuwa wafungwa ishirini na mbili (22) kati y ao
wameachiliwa huru leo tarehe 09 Disemba, 2025 na wafungwa elfu moja na kumi na nne (1,014) wamepunguziwa adhabu zao na watabaki gerezani na kuendelea kutumikia sehemu ya vifungo vilivyobaki.
“Ni matarajio ya Serikali kuwa wafungwa walioachiliwa huru leo tarehe 09 Disemba, 2025 watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.” – Waziri Simbachawene
