Nature

Wakila Kibatala Avunja Ukimya Kuhusu Hali ya  Humphrey Pole Pole

Katika kile kinachoonekana kuwa taarifa muhimu zaidi tangu kuzuka kwa sintofahamu kuhusu hatma ya Mhe. Amb. Humphrey H. Polepole, Wakili Peter Kibatala ameibuka na ujumbe mzito uliofafanua kilichotokea, kinachoendelea na kinachopaswa kupuuzwa. Kauli yake imeleta mwelekeo mpya wakati taifa likiwa bado kwenye ukungu wa maswali mengi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram wakili Kibatala amesema


“1. Kwanza kabisa, tunaomba radhi kwa ukimya uliojitokeza katika kipindi cha siku zile za giza; lakini kama nyinyi nyote mnaelewa, hizo zilikuwa siku ngumu zaidi za uwepo wetu katika nchi hii, na kipaumbele cha haraka kilikuwa ni kuishi.

Kulikuwa na amri za kutotoka nje; kukatika kwa mifumo; na mambo mengi ya giza yaliyohitaji kufutwa kutoka kwenye fikra za Taifa.

Na bado, giza la aina tofauti—ukungu wa roho—lipo. Lakini tutashinda.

  1. Pili, sisi, mawakili wake na wa familia bado tunaendelea kutoa nguvu zetu zote ndani ya mahakama. Vita kama hivi kamwe si tukio, bali ni mchakato wa mapenzi na uvumilivu. Kama ilivyo kila mara; tumeendelea kuwa wanyonge, lakini thabiti, tukijitahidi kujua hatma ya Mhe. Amb. Polepole, huku matumaini yetu yakiwa kwamba siku moja tutaungana tena.
  2. Kwa sasa, tafadhali puuzia uvumi wote uliotapakaa kuhusu kile kinachodaiwa kupatikana, baharini au kokote kule. Taarifa hizo ni za kusikitisha sana kwa familia na hazipaswi kuendelezwa.

Wale wenye nia njema wanapaswa kusubiri taarifa rasmi, na si kueneza simulizi za maumivu kwa walioathirika moja kwa moja.

  1. Nitasalia kuwa msemaji rasmi wa Familia ya Polepole katika masuala yote ya kisheria, au yanayobeba athari za kisheria.

Na kama ambavyo Humphrey mwenyewe husema kila mara:

“MUNGU WETU WA MBINGUNI AWABARIKI SANA.”


Kauli hii ya Wakili Peter Kibatala imeweka msisitizo juu ya ukweli mmoja muhimu: bado kuna safari mbele, bado kuna mapambano yanayoendelea mahakamani, na bado kuna matumaini. Wakati uvumi ukizidi kutanda mitandaoni, familia imeomba Watanzania kutulia, kusubiri taarifa sahihi na kutokubali kupelekwa na habari zisizo na uthibitisho.

Related Posts