Nature
Steven Wassira

Wasira Afunguka “Hoja ya No Reforms, No Election Haina Mashiko”

“Kwangu mimi hoja ya No Reforms, No election haina mashiko, lakini sisemi kwamba kwasababu kwangu haina na kwa wale wanaoisema ikawa haina mashiko. Labda ina mashiko lakini mimi sio msemaji wao na sielewi maana tumefanya reforms nyingi, sasa wanataka tufanye nini zaidi? Wanasema tuahirishe uchaguzi.

Haiwezekani tuahirishe uchaguzi. Uchaguzi ni Jambo kubwa na Katiba inasema hatuwezi kuahirisha uchaguzi isipokuwa kuwe na vita na vita haipo. Mashiko yapo wapi sasa maana hatuwezi kureforms zaidi kulimo tulivyofanya lakini sio kwamba ni marufuku katika siku zinazokuja na ndio maana tumesema katika Ilani yetu kuwa tutazungumza kuhusu Katiba mpya baada ya uchaguzi na huu ni ushauri tulioupata kwenye kikosi kazi cha vyama vyote isipokuwa Chadema.”- Stephen Wasira, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kwenye Dakika45 za ITV leo Julai 21, 2025.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *