Nature
Abdihamid Moallin

Watatu Yanga Watimka Haooo Kisa Kocha Mpya

Awali, Kocha mkuu wa Yanga, Romain FolzFolz alikubaliana na maombi ya mabosi wa Yanga ya kuwabakisha wasaidizi aliowakuta katika benchi la ufundi lililoachwa na mtangulizi wake Miloud Hamdi, lakini kuna mambo yamebadilika

Kuna watu watatu katika benchi la Yanga wanaondoka wa kwanza ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi, Abdihamid Moallin, mtaalamu wa uchambuzi wa mikanda ya video (video analyst), Mpho Maruping na daktari wa viungo Sekhwela Seroto.

Watatu hao wote wanatarajiwa kwenda kuungana na kocha za zamani wa Yanga, Sead Kamovic kule CR Belouzdad ya Algeria, hatua ambayo itamlazimisha Folz kurudi nyuma na kuunda upya benchi hilo kabla ya kwenda katika kambi ya maandalizi ya msimu.

Hadi sasa katika benchi hilo la Yanga, amesalia kocha wa makipa mzawa Soud Slim na kocha wa mazoezi ya viungo Taibi Lagrouni, raia wa Morocco.

Ukiacha kocha msaidizi, Folz atamleta mtaalam wa uchambuzi wa video atakayeungana na Paul Mathew ambaye ameshafika nchini, akija kuchukua nafasi ya Moallin. Folz pia anataka kufuatilia ubora wa Slim kabla ya kufanya uamuzi wa kufanya mabadiliko eneo hilo au kumuacha Slim ambaye ni kipa wa zamani wa Mtibwa Sugar.

Nafasi ya daktari wa viungo Yanga imeshaanza harakati za kumrudisha Mtunisia Youssef Ammar ambaye alikuwa katika nafasi hiyo kabla ya kuondoka alipokuja Miguel Gamondi.

Folz anataka wasaidizi hao waje mapema kabla ya timu hiyo kuondoka nchini Agosti 13 kwenda Rwanda kwa mwaliko maalum na wenyeji wao Rayon Sport watakaocheza nao mchezo

Related Posts