Taarifa za kuaminika kutoka katika chanzo cha kuaminika cha habari za michezo nchini Tanzania siku ya leo Jumatatu December 15 zinaeleza kwamba wazee wa klabu ya Simba Sc wamesoma dua ya kumuombea mambo mabaya jasusi ambaye anatajwa kuwa ni shabiki wa Yanga Sc na anafanya kazi katika klabu ya Simba Sc.
Siku za hivi karibuni afisa habari wa klabu ya Yanga Sc Ali Kamwe amekuwa na muendelezo wa kutoa taarifa mbalimbali zinazohusiana na kkabu ya Simba Sc na wakati wote amekuwa akieleza kwamba taarifa hizo amekuwa akizipata kutoka kwa mtu mmoja anayefanya kazi ndani ya klabu ya Simba Sc lakini kiuhalisia yeye ni shabiki kindakindaki wa klabu ya Yanga Sc.
Taarifa njema kwa Simba Sc, ni kwamba wazee wa klabu hiyo wamekutana siku ya leo Jijini Dar es Salaam na wamefanya dua maalumu ya kumuombea mambo mabaya jasusi huyo ambaye siku ya hivi karibuni amekuwa sehemu ya watu wanaosbabisha mgogoro mzito baina ya viongozi wa klabu ya Simba Sc na mashabiki zao.
Wazee wa klabu ya Simba Sc katika dua yao wamemuoma mwenyezi Mungu amfichue jasusi huyo kwa maana kwamba ajulikane adharani kwa mashabiki na wadau wa klabu hiyo kwani wengi wao wamekuwa na matamanio ya kumfahaku jasusi huyo.
Dua hiyo pia imelenga kumsababishia mambo mazito na mabaya jasusi huyo kwani kwa kiasi kikubwa anatajwa kuwa moja kati ya watu wanaoihujumu klabu ya Simba Sc kwa kutoa siri za klabu hiyo na kuzipeleka kwa wapinzani yaani klabu ya Yanga Sc.
Wazee wa klabu ya Simba Sc mara baada ya kumaliza dua yao, wanaendelea kusubiri majibu sahihi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na muda wowote kuanzia sasa tunaweza kushuhudia jambo jipya ndani ya klabu hiyo.
