Kufuatia kusambaa kwa video Clip zinazoonesha mvutano kati ya wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita, akiwemo Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Musukuma, Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na wajumbe wa kamati hiyo, dhidi ya mwekezaji Rashidi ambaye mkewe ni diwani wa katoro Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Riziki Shemdoe, ameingilia kati sakata hilo
Mvutano huo unahusisha mwekezaji aliyeanzisha ujenzi wa mradi katika eneo la viwanja vya CCM Katoro, Wilaya ya Geita, Mkoa wa Geita, akituhumiwa kuvamia mipaka ya eneo la kijiji/serikali na kuanzisha mradi bila kibali cha Halmashauri.
Waziri Shemdoe amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya hiyo, kufuatilia kwa kina sakata hilo na kuwasilisha majibu ndani ya siku 14
Shemdoe ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Geita katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa EPZA mjini Geita.
Kwa upande wao, Mbunge wa Jimbo la Geita Joseph Musukuma, Diwani wa Ludete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri Jumanne Misungwi, pamoja na Diwani wa Katoro ambaye mwekezaji wa eneo hilo ni mume wake — wameeleza picha ya sakata Hilo
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Afisa Ardhi Hongera Muhamedi, amesema kuwa mamlaka ya kutoa kibali cha ujenzi katika eneo hilo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kwamba Halmashauri haikutoa kibali chochote, wala chama hakijawahi kuwasilisha maombi ya kibali cha ujenzi huo kwa Halmashauri.
