
Rais William Ruto amempongeza mlinzi wa waziri mkuu wa zamani Raila Odinga , Maurice Ogeta.
Akizungumza wakati wa hafla ya mazishi ya Raila katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaramogi Oginga Odinga (JOOUST) eneo la Bondo , Kaunti ya Siaya, Rais Ruto alimhakikishia Ogeta nafasi ya kufanya kazi na serikali yake.
Ruto alikumbuka jinsi Maurice angefuta viatu vyao baada ya kampeni wakati wa siku zake katika ODM.
“Lazima tuwashukuru watu wake wa usalama. Maurice Ogeta hasa, asante sana Maurice kwa kusimama na Raila siku zote, namkumbuka Maurice enzi zetu za ODM. Huyu Maurice aliwahi kutufuta viatu tulipochelewa kutoka kwenye kampeni. Maurice nataka niwaambie serikali tunapoangalia urithi wa Raila, nanyi pia mtasimama kumwangalia Raila aliyetembea na Babaga.”

